Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Mifugo-Zanzibar

Kikao cha wadau wa Mradi wa Food Systems, Land Use and Restoration (FOLUR) kilichofanyika katika ofisi za (ZAFIRI)Maruhubi Zanzibar. kikiangazia taarifa za kitafiti na changamoto zilizopo katika mnyororo wa thamani katika zao la Mpunga.
iliyowasilishwa na Mshauri elekezi Mr Salum Faki Hamad kutoka Tasisi ya utafiti wa kilimo na Mifugo (ZALIRI).

ambapo Wadau walipata nafasi ya kujadili kwa kina hatua za kuchukua ili kuimarisha utekelezaji wa mradi, kuhakikisha matumizi bora ya mbegu ,pembejeo na matumizi ya maji ili kuongeza tija katika kilimo cha Mpunga, Aidha walikubaliana kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha malengo ya mradi huo yanatimia kwa manufaa ya jamii na maendeleo ya Taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *